Juisi Ya Ukwaju


Mahitaji:
-Maji ya moto lita moja
-Ukwaju wa kutosha
-Jagi au birika lenye uwezo wa kutosha maji lita moja au zaidi



Weka maji yako ya moto kwenye jagi au birika lako kisha weka ukwaju ndani yake (ukwaju uliotolewa maganda). 
Acha ukwaju ndani ya maji ya moto kwa muda hadi maji yatakapopoa kabisa. Baada ya hapo koroga mchanganyiko huo hadi uhakikishe kuwa juisi imekuwa nzito. 
Kisha mimina juisi yako kwenye jagi lingine kuchuja mabaki ya ukwaju (usichuje juisi kwa chujio la chai). 
Baada ya hapo juisi yako itakuwa tayari kutumika.

Comments