Juice Ya Embe


Mahitaji
1. Maembe
2.sukari
3. Tangawizi
5. Hiliki

HATUA

1. Chemsha maji ya kutosha mf lita 2 hadi 5 kulingana na wingi wa matunda

2.chukua matunda yako na uyaoshe vizuri kwa kutumia maji ya vuguvugu yaliyowekwa chumvi kiasi ili kuua vijidudu

3. Menya matunda yako taratiibu bila kujikata vidole

4.katakata matunda katika vipande vidogo vidogo ili kuiwezesha blender yako kusaga matunda kwa urahisi.

5.chukua matunda, Hiliki na tangawizi kisha weka katika brenda na anza kusaga.
Unaweza kuongeza maji yaliyochemshwa wakati wa kusaga ili kupata mchanganyiko wa wastani usio mzito sana.

6. Chukua maji yaliyochemshwa changanya na rojo la matunda kwa kiasi kulingana na wingi wa matunda kisha koroga.

7. Chukua chujio safi na chuja mchanganyiko wako huo. 

8. Chukua sukari na uitie katika mchanganyiko wako. Kisha koroga hadi sukari yote iyeyuke.

9. Chukua chombo safi maalum cha kuwekea juice na anza kuitia juice katika vyombo hivyo mf. Chupa za plastiki

10. Weka juice yako katika friji. Unaweza kunywa juice yako.

Comments