JUISI YA TIKITI MAJI NA LIMAO

MAHITAJI

5 kg ya Watermelon
180gram juice ya limao 
80 gram ya asali mbichi
1 fungu majani ya Mint
vipande vya barafu au Ice Cubes,

JINSI YA KUTENGENEZA
1.    Kata kata watermelon katika vipande vidogo, menya ngozi na kumbuka kutoa mbegu.
2.    Chukua vipande vya watermelon saga pamoja na juice ya limao
3.    Kisha ichuje katika chujio safi baada ya kuisaga
4.    Kisha weka ice cube pamoja na majani ya mint katika jagi.
5.    Kisha mimina juice katika jagi lako lenye barafu na mint
6.    Kisha mimina asali mbichi kwenye mchanganyiko wa juisi na ukoroge ichanganyike.

Comments