JUISI YA PAPAI


MAHITAJI

480 gram papai lililoiva ( sawa na papai moja lililoiva)
240 gram sukari
1 juisi ya limao au ndimu kijiko kikubwa cha chakula ( sawa na malimao au ndimu 2 - 3)
480 gram maji safi ya baridi

Jinsi ya kuandaa
Menya papai kisha tumia kijiko kuondoa mbegu na utando wa juu unaoshikilia hizo mbegu, kisha kata katika vipande vidogo vidogo.

Kisha chukua papai, sukari, juisi ya limao au ndimu na maji saga katika blender pamoja na kisha weka katika friji ipoe.

PIA UNAWEZA WEKA PILI PILI MANGA KIASI SIO LAZIMA NI KATIKA KUONGEZA LADHA.

Comments