Juisi Ya Embe

Maembe yaliyoiva - 2
Mtindi (yogurt) - 2 Vikombe vya chai
Maziwa - 1 Kikombe cha chai
Asali au Sukari - ¼ Kikombe cha chai
Maji ya ndimu - ½ Kipande
Barafu - 12 vipande
Mdalasini ya unga - kidogo


Namna Ya Kutayarisha
1.    Ambua maembe kisha ukate kate vipande.
2.    Weka vipimo vyote isipokuwa mdalasini, kwenye mashine ya kusagia (blender).
3.    Saga hadi ilainike.
4.    Mimina kwenye gilasi na unyunyize mdalasini na itakuwa tayari.

Comments